Dodoma FM

Visima Nzuguni vitaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 75

3 April 2023, 6:05 pm

Zoezi la uchimbaji Visima Nzuguni likiwa linaendelea . Picha na Mindi Joseph.

kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2022 idadi ya watu katika Mkoa wa Dodoma imeongezeka kutoka milioni 2.085 ya mwaka 2012 hadi milioni 3.085, ongezeko hilo limekuja na upungufu wa huduma mbalimbali ikiwemo ya maji.

Na Mindi Joseph.

Kukamilika kwa Uchimbaji wa visima vya maji katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma imetajwa kuongeza kiwango cha upatikanaji maji kutoka asilimia 50.8 ya sasa hadi asilimia 75.

Taswira ya habari imefanya mahojiano na Mwenyekiti wa mtaa wa Nzunguni A Onaely Mbatiani amesema upatikanaji wa maji bado ni changamoto licha ya kuwa na visima 4 vinavyochimbwa ambavyo vinatarajiwa kukamilika mwezi wa Nane.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Nzunguni A Onaely Mbatiani
Zoezi la uchimbaji Visima Nzuguni likiwa linaendelea . Picha na Mindi Joseph.

Kwa upande wao wananchi wa Mtaa wa Nzunguni A wamesema haya.

Sauti za wananchi wa Nzuguni A