Dodoma FM

Jamii yatakiwa kusaidia watoto wenye usonji

3 April 2023, 12:24 pm

Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma  Prof Davis Mwamfupe akiwa kwenye tukio ambalo limewahusisha watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi mlezi jijini Dodoma.Picha na Seleman Kodima.

Kuna haja ya kuwajumuisha watu wenye ulemavu ikiwemo wenye usonji ili kutimiza azma ya Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs ya kutomuacha yeyote nyuma.

Na Seleman Kodima.

Jamii imetakiwa kushirikia kikamilifu kusaidia kutatua changamoto zote zinazowakumba watoto wenye usonji bila kutazama ni mtoto wa nani na anatoka wapi .

Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma  Prof Davis Mwamfupe wakati akizungumza na wadau ,walimu na wazazi kwenye tukio ambalo limewahusisha watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi mlezi jijini Dodoma kwenye bonanza la michezo .

Mstahiki Meya Prof Davis Mwamfupe amesema kuwa tabia ya jamii kumuachia mzazi wa mtoto mwenye usonji pekee ni hali mbaya yenye kuongeza changamoto zenye kushindwa kutatuliwa na jamii yenyewe.

Sauti ya Mstahiki Meya Prof Davis Mwamfupe

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi -Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt  Omary Ubuguyu amesema lengo la wadau kufika shuleni hapo ni kuongeza hamasa kwa jamii na kuwakumbusha kuwa wananafasi ya kusaidia kutatua changamoto zinazowakumbua watoto hao .

Sauti ya Mkurugenzi Msaidizi -Magonjwa yasiyoambukiza Dkt  Omary Ubuguyu

Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma  Prof Davis Mwamfupe akipeana mikono na watoto Picha na Seleman Kodima.

Nae Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlezi Mwl  Anicetus Lyimo akisoma risala fupi kwa Mgeni Rasmi na wageni amebainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili kitengo cha elimu maalumu ikiwa ni pamoja na usalama wa watoto wakati kucheza kutokana na ukosefu wa uzio katika shule hiyo

Sauti ya Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mlezi Mwl  Anicetus Lyimo

Pamoja na hayo katika bonanza hilo wanafunzi hao walishiriki michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu,riadhaa na kupewa zawadi tofauti ikiwa ni ishara ya kuwathamini na kuonesha umuhimu wao kwenye jamii hali ambayo  inabeba malengo ya dunia.  .