Dodoma FM

CCM Bahi haijaridhishwa na Ujenzi wa kituo cha mabasi

3 April 2023, 5:02 pm

kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilayani humo iliyotembelea na kukagua zaidi ya miradi 26 ya maendeleo. Picha na Bernad Magawa.

kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ccm wilayani humo imetembelea na kukagua zaidi ya miradi 26 ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya, elimu, maji, na miundombinu ya barabara ili kuona namna ILANI ya ccm inavyotekelezwa.

Na Benard Magawa.

Chama cha Mapinduzi wilayani Bahi kimeeleza kutoridhishwa naUjenzi wa stendi ya mabasi wilayani humo huku kikipongeza baadhi ya miradi inavyotekelezwa kwa ufanisi na kuiagiza serikali kuona namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kuhusu Stendi hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima katika ziara ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilayani humo iliyotembelea na kukagua zaidi ya miradi 26 ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya, elimu, maji, na miundombinu ya barabara ili kuona namna ILANI ya ccm inavyotekelezwa.

Masima amesema hajaridhishwa na thamani ya fedha zilivyotumia kujenga stendi hiyo pamoja na utendaji wake kwani wananchi wanapata adha kubwa ikiwepo ongezeko la nauli mara dufu kutoka Bahi mpaka Dodoma mjini kuliko viwango vya nauli kabla ya stendi hiyo.

Aidha ameipongeza serikali kuhusu ujenzi wa vituo vya huduma za afya na madarasa na kuagiza majengo yote kukamilishwa kwa wakati ili yaanze kutoa huduma kwa wananchi huku akishauri serikali kuhakikisha watumishi wanapatikana kwa wakati.

Kuhusiana na Miradi ya Barabara Mwenyekiti huyo ameeleza kamati kuridhishwa na uimara wa mtandao wa barabara wilayani Bahi na kutoa pongezi kwa wakala wa Barabara vijijini ( TARURA) kwa kuwa na ujenzi imara kuliko ilivyokuwa awali.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bahi Stuwart Masima

Naye kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Honolina Mnkunda ambaye aliambatana na kamati ya siasa pamoja na wakuu wa idara mbalimbali amesema serikali itayafanyia kazi maagizo ya chama kadiri maelekezo yalivyotolewa.

Sauti ya kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Honolina Mnkunda

Kwa upande wao baadhi ya madereva wa magari ya abiria yanayofanya safari za Bahi Dodoma na madereva bodaboda nao wakaeleza changamoto zao kuhusu stendi hiyo huku abiria wakiiomba serikali kuruhusu abiria kupanda na kushuka eneo la awali ili kupunguza makali ya nauli.

Sauti za madereva wa magari ya abiria yanayofanya safari za Bahi Dodoma