Dodoma FM

Zaidi ya wananchi 2249 wapatiwa elimu ya kujikinga na MARBURG

30 March 2023, 6:52 pm

Mtalaam wa Ufuatiliaji wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Emmanuel Mwakapasa. Picha Mindi Joseph.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kufikia makundi mbalimbali ya watu ikiwemo  wahudumu wa afya  ngazi jamii  na Wahudumu wa Afya Vituoni.

Na Mindi Joseph.

Elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Marburg imeendelea kutolewa kwa  kila mtanzania tangu itolewe taarifa ya ugonjwa huo huku zaidi ya wananchi  2249  wamefikiwa na Elimu Nchini.

Taswira ya Habari imezungumza na Mtalaam wa Ufuatiliaji wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Emmanuel Mwakapasa ambapo amesema.

Sauti ya Mtalaam wa Ufuatiliaji wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya, Emmanuel Mwakapasa

Katika hatua nyingine Mwakapasa ametaja dalili za Ugonjwa huo.

Baadhi ya wananchi wakipatiwa elimu ya jinsi ya kujikinga na Marburg.Picha na Mindi Joseph.
Sauti ya Mtalaam wa Ufuatiliaji wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya,

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa huo uligundulika kwa mara ya kwanza Ujerumani mwaka 1967 na ndio asili ya jina la ugonjwa huu na ulishawahi kutolewa taarifa katika nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya .