Dodoma FM

Katibu mkuu aridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi

30 March 2023, 5:34 pm

Ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa maeneo yenye miradi ya ujenzi.Picha na Martha Mgaya

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo.

Na Seleman Kodima.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi inayosimamiwa na Ofisi hiyo na kwamba kukamilika kwake kutawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa maeneo yenye miradi ya ujenzi iliyopo chini ya Ofisi hiyo na kuwataka wakandarasi kuongeza juhudi ili majengo hayo yakamilike kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Amesema uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutekeleza miradi hiyo mikubwa ni kuhakikisha shughuli za Serikali zinafanyika katika mazingira yenye ubora na kuhudumia wananchi kwa weledi.

Sauti ya Dkt. Yonazi.

Kwa upande wake Mkadiriaji Majenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Mhandisi Saudeni Anania ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana nao huku akieleza changamoto wanayokabiliana nayo kwa sasa ni upungufu wa vifaa vya umaliaziaji wa ujenzi.

Sauti ya Mkadiriaji Majenzi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Mhandisi Saudeni.

Katika ziara hiyo katibu mkuu dkt. Jim yonazi amewahimiza wakandarasi kuhakikisha wapata vifaa kwa wakati ili ujenzi huo uweze kufanyika ndani ya muda uliopangwa pamoja na wasimamizi kusimamia kikamilifu kuhakikisha majengo hayo yanakuwa na ubora unaotakiwa.