Dodoma FM

WAUVI yazindua mafunzo kwa wajasiriamali 500 Dodoma

28 March 2023, 2:00 pm

Baadhi ya wajasiriamali hao wakiwa katika uzinduzi wa mafunzo hayo ulio fanyika hapo jana. Picha na Alfred Bulahya.

Mafunzo hayo yamezinduliwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo bi Habiba Ryengite yatakaohusisha wanawake 400.

Na Alfred Bulahya

Taasisi ya Wanawake na uchumi wa viwanda WAUVI imezindua mafunzo kwa wajasiriamali 500 Jijini Dodoma kwa ajili ya kuwawezesha kutengeneza bidhaa zenye ubora thabiti pamoja na kuanzisha viwanda.

Mafunzo hayo yamezinduliwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo bi Habiba Ryengite yatakaohusisha wanawake 400 huku wanaume wakiwa 100 na kwamba yatatolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO.

Baadhi ya wajasiriamali hao wakiwa katika uzinduzi wa mafunzo hayo ulio fanyika hapo jana. Picha na Alfred Bulahya.

Akizungumza na Taswira ya habari baada ya kuzindua mafunzo hayo amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutengeneza bidhaa na viwanda maalumu.

Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo bi Habiba Ryengite

Aidha amewaomba wanawake wajasiriamali kuhakikisha wanaungana na kuwa kitu kimoja.

Justine Benedict Kahemela ni Msimamizi wa Fedha kutoka SIDO mkoa wa Dodoma akaeleza namna gani watashiriki katika kutoa mafunzo hayo.

Sauti ya Justine Benedict Kahemela ni Msimamizi wa Fedha kutoka SIDO

Mwenyekiti wa WAUVI mkoa wa Dodoma Rehema Said Nassoro, ameeleza malengo ya kufanya mafunzo hayo huku mlezi wa taasisi hiyo Shufaa Iddi akiwataka wanaume kuwaruhusu wake zao kujiunga na taasisi hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa WAUVI mkoa wa Dodoma Rehema Said Nassoro