Dodoma FM

Wakazi wa Dodoma wahamasishwa kutembelea vivutio vya utalii

28 March 2023, 3:58 pm

Twiga wanaopatikana katika pori la akiba Mkungunero lililopo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ili kukuza utalii katika Mkoa wa Dodoma Taasisi mbalimbali, wadau pamoja na wananchi kutembelea katika mapori hayo ya akiba.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amewataka wananchi,Taasisi pamoja wadau mbalimbali kushiriki kutembelea katika vivutio vilivyopo katika mkoa wa Dodoma ili kukuza utalii Mkoa hapa.

Mh Senyamule ameyasema hayo  wakati alipofanya ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali zenye vivutio  Ikiwemo pori la Akiba la Mkungunero ambapo alipata nafasi ya kushuhudia baadhi ya wanyama katika pori hilo wakiwemo Twiga na Tembo

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliambatana na wakuu wa wilaya za Dodoma akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh Khamis Mkenachi na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  Sophia Kizigo ambapo nao walikua na haya ya kuzungumza katika ziara hiyo.

Sauti za Wakuu wa wilaya.
Mh. Senyamule akitazama mandhari ya pori hilo la akiba Mkungunero .Picha na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.