Dodoma FM

Ilindi inatekeleza kilimo cha mtama ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

28 March 2023, 5:32 pm

Kilimo cha mtama mweupe Ilindi. Picha na Bernad Magawa.

Kilimo cha mtama mweupe ambao umekuwa ukihamasishwa na viongozi mbalimbali wilayani Bahi kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Na Bernad Magawa

Wakulima wa kijiji cha Ilindi wialayani Bahi wameanza kutekeleza kwa vitendo suala la kilimo cha
mtama mweupe ambao umekuwa ukihamasishwa na viongozi mbalimbali wilayani humo kwa
lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuongeza pato la wakulima kupitia zao hilo
ambalo linastawi katika maeneo yenye mvua kidogo.

Akieleza mapokeo ya kilimo hicho Mwenyekiti wa kijiji cha Ilindi Peter Mtundu amesema kilimo
cha mtama hakikuwa kipaumbele kwa wakulima wengi hapo awali lakini kwa sasa
wamehamasika kulima baada ya kuelimishwa huku akitoa shukrani kwa viongozi waliowezesha
kuanza kwa kilimo hicho huku nao baadhi ya wananchi wakieleza namna walivyohamasika
kulima mtama mweupe.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Ilindi Peter Mtundu

Kwa upande wa wakulima wanao lima kilimo hicho cha mtama wao wanasema.

Sauti ya Christina Julias Mkulima.
Shamba la mtama Mweupe. Picha na Benard Madawa

Akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo wa Ireland Mheshimiwa Peppa Hachet
aliyoifanya mapema Mwezi huu kwenye kata ya Ilindi kwa lengo la kujionea na kuhamasisha
kilimo cha mtama mweupe, Mbunge wa Jimbo la Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo ametoa rai
kwa wananchi kuchangamkia kilimo hicho ili kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Bahi Mheshimiwa Kenneth Nollo

Kilimo cha mtama mweupe wilayani Bahi ni zao ambalo linaelekea kuwa mkombozi kwa
wananchi kujihakikishia uhakika wa chakula huku shirika la Chakula Duniani na mashirika
mengine yakitajwa kuwa wateja wakuu wa zao hilo.