Dodoma FM

Wananchi Kondoa wasisitizwa kilimo cha umwagiliaji

27 March 2023, 2:20 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwataka wananchi wa Wilaya ya Kondoa kujikita katika kilimo Cha Umwagiliaji Ili kuondoa Janga la njaa.Picha na ofisi ya mkuu wa mkoa

Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Wilaya ya Kondoa kujikita katika kilimo Cha Umwagiliaji Ili kuondoa Janga la njaa, kujiongezea kipato na kukabiliana na mabadiliko ya tabi ya nchi.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Wilaya ya Kondoa kujikita katika kilimo Cha Umwagiliaji Ili kuondoa Janga la njaa, kujiongezea kipato na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Mhe Rosemary ametoa wito huo wakati alipokua akizungumza na wananchi wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wafanyabiashara na kusisitiza kutopandisha bei ya vyakula kwenye kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.