Dodoma FM

Wadau wa Elimu watakiwa kutumia mipango kazi kuleta mapinduzi

27 March 2023, 2:47 pm

Wadau wa Elimu wakiwa katika mkutano huo.Picha na Selema Kodima.

Baadhi ya wadau wa elimu na viongozi wa serikali za mitaa katika kata nne za halmashauri ya wilaya ya chamwino walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo kumekuwa na matokeo chanya..

Na Seleman Kodima.

Wadau wa Elimu wilayani Chamwino wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kupitia mipango kazi wanayoanda ili kusaidia kuleta mapinduzi katika utoaji wa elimu bora kuanzia Ngazi ya kata hadi kijiji

Hayo yamesemwa na Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Chamwino Merry Muhoza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyowakutanisha Wadau wa Elimu wakiwamo maafisa elimu kata, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji  na wawakilishi kamati za ufatiliaji na uwajibika za mitaa yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AFNET na kufanyika jijini Dodoma,

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Chamwino Merry Muhoza .

Muhoza amewaomba AFNET kushirikiana na serikali kupitia kamati za MTAKUWA katika kuwajengea uwezo ili  kusaidia kuongeza uelewa kwa wanajamii hao juu ya vitendo vya ukatili wa jinsia.

Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Chamwino Merry Muhoza .
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Chamwino Merry Muhoza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu

Nae Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET bi Joy Njelango amesema kupitia mafunzo hayo wanatarajia kuona ushirikiano baina ya watawala na ngazi zote katika ufatiliaji na utatuzi wa changamoto zote zilizopo katika sekta ya elimu

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET bi Joy Njelango

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo hayo Sudi Mazege    amewataka washiriki wote kwenda kutekeleza kwa vitendo mafunzo hayo na kuhakikisha wanasimamia mpango kazi waliojiwekea ili kufanikisha malengo.

Mwenyekiti wa mafunzo hayo Sudi Mazege . Picha na Seleman Kodima.

Baadhi ya wadau wa elimu na viongozi wa serikali za mitaa katika kata nne za halmashauri ya wilaya ya chamwino walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo kumekuwa na matokeo chanya kuanzia ngazi za vijiji ikiwemo uwepo wa kamati za uwajibikaji,ufatiliaji  na kuhamaisha jamii kuhusu elimu bora.