Dodoma FM

UCSAF yatoa mafunzo ya Tehama kwa wasichana shule za sekondari Nchini

23 March 2023, 11:26 am

Badhi ya wanafunzi wa Kidato cha tatu Shule za Sekondari nchini wakiwa  katika ufunguzi wa Mafunzo ya TEHAMA. Picha na full shangwe.

Itakumbukwa kuwa siku ya kimataifa ya msichana katika TEHAMA inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 27 April  lengo likiwa ni  kuchochea harakati za dunia katika kuongeza idadi ya wasichana na wanawake kwenye nyanja ya teknolojia.

Na Mariam Matundu.

Katika kuelekea siku ya wasichana katika tehama mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF umetoa mafunzo yaliyoenda sambamba na mashindano ya tehama kwa wasichana katika shule za sekondari hapa nchini .

Wasichana walishiriki mafunzo hayo kwa siku nane na kisha kubuni mifumo ya tehama inayoleta suluhu ya mambo katika jamii ambapo wamesema tehema ni muhimu kwa wasichana na imewasaidia kuleta motisha ya kupenda tehama .

Sauti ya Wasichana walishiriki mafunzo hayo

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF PROF John Mkoma amesema lengo la mafunzo na mashindano hayo ni kuendelea kuwawezesha wasichana katika mawasiliano na tehama .

Sauti ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF PROF John Mkoma
Badhi ya wanafunzi wa Kidato cha tatu Shule za Sekondari nchini wakiwa  katika ufunguzi wa Mafunzo ya TEHAMA. Picha na full shangwe.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ,Naibu waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari mhandisi Kundo Mathew amesema serikali imekuwa ikifanyia kazi sera na sheria mbalimbali ili kuifanya Tanzania  kuwa moja ya nchi zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Sauti ya Naibu waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari mhandisi Kundo Mathew

Aidha amewahakikishia wanafunzi hao wasichana waliobuni mifumo mbalimbali ikiwemo wa kuthibiti utoro shuleni (MAHUDHURIO APP) mfumo wa kuripoti ukatili (GENDER BASE VAOLENCE APP)na mfumo wa kusaidia lishe bora (TOTO LISHE APP) kwenda kuwasilisha application zao kwa mawaziri wenye dhamana ikiwemo Tamisemi na Maendeleo ya jamii.

Jumla ya wanafunzi 246 wasichana kutoka shule mbalimbali za sekondari katika mikoa yote ya tanzania bara na Zanzibar walipatiwa mafunzo katika vituo vya chuo kikuu cha dodoma UDOM,chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya MUST,pamoja na Dar es salaam institute of technology DIT ambapo washindi 31 kutoka mikoa yote wamepatikana na kupatiwa mafunzo yaliyowezesha kubuni Aplication tatu .