Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuendelea kupata elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji

22 March 2023, 6:54 pm

Mkutano wa Uzinduzi wa Mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu 2023 -2027. Picha na Mindi Joseph.

Tanzania ilishuhudia kipindi kirefu cha mlipuko wa Kipindupindu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2018 na Taarifa kutoka shirika la Afya Dunia inaeleza kuwa na mlipuko mkubwa wa Kipindupindu nchini Malawi ambapo hadi kufikia tarehe 15 Machi 2023 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 53,925 na vifo 1,658.

Na Mindi Joseph.

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu Sera Mbuge na Uratibu Mh George Simbachawene amezitaka Ofisi za Serikali za Mikoa na Halmashauri kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kuoga, kufua pamoja na kutupa takataka ovyo.

Ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu 2023 -2027.

amesema mpango huo unalenga kuhakikisha kuwa ugonjwa huu kwanza unazuiwa lakini pia unakabiliwa pale utakapokuwa umevuka mipaka na kuingia Nchini.

Sauti ya Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu Sera Mbuge na Uratibu Mh George Simbachawene

Katibu mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu Sera Mbuge ma Uratibu Jin Yonaz anasema Mpango huo unalenga kupunguza ugonjwa wa kipindupindu kwa asilimia 90.

Sauti ya Katibu mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu Sera Mbuge ma Uratibu Jin Yonaz

Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir shekimweri amesema uzinduzi wa mpago huu umekuja wakati.sahihi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir shekimweri.