Dodoma FM

Wananchi Bahi waomba kupunguziwa gharama za kuunganishiwa umeme

22 March 2023, 7:23 pm

Mhandisi King Fukanya Meneja Tanesco Wilaya ya Bahi hapo juu.Picha na Benard Magawa

Wananchi wilayani Bahi wameliomba shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuwapunguzia gharama za kuunganishiwa umeme kwa matumizi ya nyumbani.

Na Benard Magawa.

Wananchi wilayani Bahi wameliomba shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuwapunguzia gharama za kuunganishiwa umeme kwa matumizi ya nyumbani kutoka zaidi ya 300,000/= bei ya sasa hadi shilingi 27,000/= bei ambayo ilikuwa ikitumika hapo awali inayoelezwa kuwa iliwasaidia wananchi wa kipato kidogo kuunganishiwa nishati hiyo.

Akitoa ombi hilo kwa TANESCO mmoja wa mafundi umeme wilayani humo Bwana Michael Mlelwa amesema tangu kupanda kwa gharama za kuunganishiwa umeme mafundi wengi wamekosa kazi kwani wateja wao wengi hawawezi kumudu gharama hizo.

Amesema japo Bahi ni makao makuu ya wilaya lakini bado mazingira yake na mfumo mzima wa utoaji wa huduma za jamii unaendeshwa kwa mfumo wa kijiji na siyo mji hivyo kwa mujibu wa miongozo ya Tanesco Bahi bado panastahili kuunganishiwa umeme kwa gharama za kijijini.

Saauti ya Bwana Michael Mlelwa.

Meneja wa Tanesco wilaya ya Bahi Mhandisi King Fokanya amesema tayari alishapokea maagizo kutoka Makao makuu ya shirika yakimuelekeza kuainisha maeneo yote ambayo bado ni vijiji lakini kwa bahati mbaya yamejikuta yakihudumiwa kwa mfumo wa miji, huku akifafanua bei elekezi za kuunga umeme kwa wateja kwenye maeneo tofauti tofauti na kuahidi kufuatilia kwa haraka suala hilo.

Sauti ya meneja wa Tanesco wilaya ya Bahi Mhandisi King Fokanya.