Dodoma FM

Vijana waomba viongozi kutembelea maeneo yao ya kazi

22 March 2023, 7:02 pm

Baadhi ya shughuli ya kuponda kokoto katika mtaa wa kisasa Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli ya kuponda kokoto katika mtaa wa kisasa Dodoma wametoa ushauri kwa viongozi mbalimbali kutembelea maeneo yao ya kazi.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli ya kuponda kokoto katika mtaa wa kisasa Dodoma wametoa ushauri kwa viongozi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kuwatembelea vijana katika maeneo yao ya kazi ili kufahamu zaidi changamoto zinazowakabili.

Hayo yamesemwa na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli ya kuponda na kuuza kokoto katika mtaa wa kisasa wakati dodoma tv ilipowatembelea na kusema ni kwa kiasi gani shughuli hizo zinavyowasaidia kujipatia kipato na changamoto zinazowakabili.

Sauti za wafanyabiashara.

wameongeza kuwa ni vyema serikali kuweka utaratibu wa viongozi kuwatembelea katika maeneo mbalimbali wanayofanyia shughuli zao ili kubaini iwapo zipo changamoto na kupata ushauri wa ni kwa namna gani wanaweza kunufaika zaidi.

Sauti za wafanyabiashara.

Vijana hao wanasema kuwa eneo hili la kisasa limesaidia wastani wa vijana kati ya 100 hadi vijana 200 kupata fursa ya kujiajiri katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na shughuli ya kuponda kokoto.