Dodoma FM

Serikali yadhamiria kudhibiti na kutokomeza kifua kikuu

22 March 2023, 3:46 pm

kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya waziri Mkuu.

Immelezwa kuwa watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu(TB)  ni pamoja na wale wanaoishi katika makazi duni, Watoto, Wavuvi na  wanafunzi wanaoishi bweni.

Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi katika  kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Sauti ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi

Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri kutoka Stop TB Partnership (STP) Bw. Oscar Mukasa wakati akiwasilisha taarifa ya mpango kazi wa kudhibiti Kifua Kikuu amesema watu wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo  ni pamoja na wale wanaoishi katika makazi duni, Watoto, Wavuvi na  wanafunzi wanaoishi bweni.

Sauti ya Mtaalamu Mshauri kutoka Stop TB Partnership (STP) Bw. Oscar Mukasa

Aidha Bw. Mukasa amewashauri watu wanaoishi katika mazingira Duni kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kwa kufuata maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya.