Dodoma FM

Wahandisi wa SGR watakiwa kusimamia fidia za wananchi

21 March 2023, 5:06 pm

W.ananchi ambao bado hawajapata malipo ya maeneo yaliyochukuliwa na mradi na kuagiza wananchi.Picha na Bernad Magawa

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Gondwe ametoa maelekezo kwa wahandisi wanaosimamia mradi wa reli ya treni ya Mwendo kasi kuhakikisha wanashughulikia kero wananchi ambao hadi sasa hawajalipwa fidia za ardhi.

Na Bernad Magawa.

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Gondwe ametoa maelekezo kwa wahandisi wanaosimamia mradi wa reli ya treni ya Mwendo kasi kuhakikisha wanashughulikia kero wananchi ambao hadi sasa hawajalipwa fidia za ardhi waliyoitoa kwa shirika hilo kwaajili ya kupisha ujenzi wa mradi huo wa kitaifa unaoendelea kujengwa hapa nchini.

Gondwe ameyasema hayo baada ya kutembelea na kuzungumza na wananchi ambao bado hawajapata malipo ya maeneo yaliyochukuliwa na mradi huo na kuagiza wananchi wote wanaolidai shirika hilo kuorodheshwa majina yao na kupelekwa Ofisini kwake ili wahakikiwe na kufuatiliwa fidia zao.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Gondwe.

Amesema mradi wa SGR ni fursa kubwa kwa watanzania kwani umeajiri vijana wengi na kuahidi kuzungumza na Uongozi wa TRC kuomba treni iweze kusimama walau kwa dakika nyingi kwenye stesheni ya Bahi ili wananchi waweze kufanya biashara za ambazo zitawaimarisha kiuchumi.

Awali baadhi ya wananchi wilayani Bahi ambao wengi wamechukuliwa maeneo yao ya mashamba wameeleza kero ya kutolipwa fidia za maeneo yao kwa muda mrefu na kumuomba Mkuu wa wilaya hiyo kuwasaidia ili waweze kupata haki zao .
Akieleza kwa niaba ya wananchi kuhusiana na kadhia hiyo mzee Matonya ambaye ni mkazi wa kijiji cha

Nagulo kata ya Bahi amesema walioandikishwa awamu ya kwanza tayari walishalipwa lakini baada ya hapo bado hakuna aliyepewa fidia na wamefuatilia kwa muda mrefu kuhusu kulipwa haki zao lakini hadi sasa bado hawajapata.

Sauti ya mzee Matonya.

Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa wilaya zilizopitiwa na mradi mkubwa wa kitaifa wa treni ya mwendo kasi ambao unaendelea kujengwa hapa nchini.