Dodoma FM

Dkt. Mollel azungumza na wataalamu wa Afya.

21 March 2023, 5:39 pm

Wahudumu wa Afya wakiwa katika maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Afya.

Amewapongeza watoa huduma wote kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi licha ya changamoto wanazokutana nazo, huku akiweka wazi kuwa, Serikali itaendelea kuboresha maslahi yao.

Na Pius Jayunga.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka Wataalamu wa Afya kutomchukia pindi anapofanya maamuzi ya kumtoa Mganga Mkuu wa Wilaya kwani hufanya hivyo kwa nia njema ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Dkt. Mollel ametoa wito huo alipomwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Sauti ya Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel.

Sambamba na hilo Dkt. Mollel ametoa wito kwa Wataalamu hao kuunga mkono jitihada za Serikali za kuja na Sheria ya Bima ya afya kwa woteitayotoa fursa kwa wananchi kupata matibabu katika hospitali yoyote nchini kuanzia zahanati mpaka taifa.

Sauti ya Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel.