Dodoma FM

Wazazi waliokatisha watoto masomo kukamatwa

17 March 2023, 4:04 pm

Picha ya waziri wa Elimu Adolf Mkenda. Picha na Huheso digital.

Baadhi ya wazazi wanadai elimu zote mbili zina umuhimu huku wengine wakibainisha kuwa  walimu pia wanachangia kuongeza kwa  utoro shuleni.

Na Nizar Khalfan.

Zoezi la ukamataji la wazazi wa wanafunzi watoro limeanza wilayani kondoa ambapo zaidi ya wazazi kumi na mbili wamekamatwa huku wakidaiwa kuwaachisha wanafunzi hao masomo   na kuwapeleka madrasa kujifunza elimu ya Dini

Wakizungumza na dodoma fm Baadhi ya wakazi wa wilaya ya KONDOA wamesema elimu zote mbili zina umuhimu huku wengine wakibainisha kuwa  walimu pia wanachangia kuongeza kwa  idadi ya utoro shuleni

Sauti za baadhi ya wazazi

Nae mtendaji wa kata ya KONDOA mjini Samson Godfrey Mtui amesema zoezi Hilo limeanza na tayari zoezi la kuwapeleka wazazi hao mahakamani huku watoto hao wametakiwa kuanza  kuhudhuria Masomo kuanzia march 28 mwka huu.

Sauti ya mtendaji wa kata ya KONDOA mjini Samson Godfrey Mtui .