Dodoma FM

Wananchi kulipwa fidia ya bilioni 10 kupisha ujenzi wa barabara Ntyuka

17 March 2023, 4:34 pm

Baadhi ya Wajumbe wa bodi wakifatilia mkutano huo.Picha na Mariam Kasawa.

Barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami  inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 38 na  hadi kufikia mwezi Feburuary ujenzi umefikia asilimia 4.

Na Mindi Joseph.

Jumla ya wananchi 1522 Mkoani Dodoma wanatarajiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 10 ili kupisha Ujenzi wa Barabara ya Ntyuka Mvumi hadi Kikombo yenye urefu wa kilometer 25.

Ameyasema hayo  jijini Dodoma Mkuu wa matengenezo TANROAD Mhandisi Salome Kabunda wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023.

Sauti ya Mkuu wa matengenezo TANROAD Mhandisi Salome Kabunda

Kwa uapnde wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary  Senyamule amehimiza ufuatiliaji wa barabara ya Mpunguzi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary  Senyamule

Naye Mbunge wa Bahi Mh Keneth Nollo amesema milion 900 zinatumiaka katika ujenzi wa barabara ya Mpunguzi.

Sauti ya Mbunge wa Bahi Mh Keneth Nollo

Kikao cha Bodi ya Barabara kimefanyika leo jijini Dodoma kikiwakutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili utekeleza wa bajeti ya mwaka 2023