Dodoma FM

Miaka miwili bila Magufuli wananchi waendelea kumuenzi

17 March 2023, 5:30 pm

Hayati John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania enzi za uhai wake. Picha kutoka Maktaba.

Leo imetimia miaka miwili tangu alipofariki Dunia Rais wa Serikali ya awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufu.

Na Fred Cheti.

Ikiwa leo imepita miaka miwili tangu kifo cha aliyekuwa  Rais wa  serikali ya awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli wananchi jijini hapa wameeleza jinsi wanavyo muenzi na kuukumbuka mchango wa kiongozi huyo kwa Taifa..

Wakizungumza na Dodoma Tv kwa nyakati tofauti wananchi hao wameonesha kumkumbuka kwa mengi mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Sauti za Wananchi.

Aidha wananchi hao wametoa ushauri kwa viongozi mbalimbali wa sasa kuiga moyo wa uzalendo na wa kuwatumikia wananchi kama aliokua nao hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Sauti za Wananchi.

Dkt Magufuli alizaliwa Wilayani Chato Mkoani Geita mnamo Oktoba 29, 1959 na aliaga dunia Machi 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam na kuzikwa Machi 26 nyumbani kwake Chato mkoani Geita..