Dodoma FM

Juhudi za serikali kuinua kilimo na wakulima wa zabibu Dodoma

17 March 2023, 4:27 pm

Serikali kupitia wizara ya kilimo imeanza kulifufua shamba la Zabibu lililopo eneo la Chinangali 2 mkoani Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Serikali kupitia wizara ya kilimo imeanza kulifufua shamba la Zabibu lililopo eneo la Chinangali 2 mkoani Dodoma, ufufuaji wa shamba hilo unakwenda sambamba na ujenzi wa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata zabibu hizo.

Na Alfred Bulahya.

Serikali kupitia wizara ya kilimo imeanza kulifufua shamba la Zabibu lililopo eneo la Chinangali 2 mkoani Dodoma ikiwa ni jitihada za kukiinua kilimo na wakulima wa zabibu Mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa wakulima wa Zabibu Mkoani Dodoma Bw, David Mtimbi Mwaka, wakati akizungumza katika kipindi cha The Morning Power Show.

Akiwa katika kipindi hicho amesema ufufuaji wa shamba hilo unakwenda sambamba na ujenzi wa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata zabibu hizo ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Sauti ya Bw, David Mtimbi Mwaka.

Ufufuaji wa shamba na ujenzi wa kiwanda hicho unatajwa kuwa kusaidia wakulima wa zao hilo kuuza zabibu katika soko la kimataifa kwa kuuza zabibu ghafi.