Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuhimiza watoto kusoma

15 March 2023, 6:06 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.Picha na Martha Mgaya

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wazazi na walezi kutumia fursa za vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu zilizopo mkoani Dodoma.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wazazi na walezi kutumia fursa za vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu zilizopo mkoani Dodoma kwa kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii na kuepusha utoro shuleni ili waje watumie nafasi za kusoma katika vyuo hivyo.

Mhe. Rosemary ameyasema hayo wakati akizungumza na wazazi na walezi wa kata ya Chang’ombe baada ya kumalizika kwa tukio la upandaji miti katika shule ya Msingi Chang’ombe B iliyopo jijini hapa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

Katika hatua nyingine Mh. Rosemary ameitaka jamii kuepuka matukio ya ukatili wa kijinsia mabayo kwa sasa yamekua yakithiri katika jamii na kumtaka kila mwananchi awe mlinizi kwa mwenzake.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.