Dodoma FM

Wananchi wajeruhiwa na wengine kupoteza makazi baada ya mvua kubwa kunyesha

15 March 2023, 4:28 pm

Nyumba zipatazo 16 zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali.Picha na Mariam Matundu

Nyumba zipatazo 16 zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali,mkoani Dodoma na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa huku wengine wakibaki bila makazi.

Na Alfred Bulahya.

Nyumba zipatazo 16 zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, katika vitongoji vya Milima mitatu, Kawawa, Mwenge, na Muungano vilivyopo kata ya Mlowa Bwani wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa huku wengine wakibaki bila makazi.

Diwani kata hiyo bw, Andrew Richard Mseya amethibitisha hilo akisema tayari wamechukua hatua za kubainisha athari zilizotoka baada ya mvua hiyo kwa ajili ya hatua zaidi.

Sauti ya Diwani kata hiyo bw, Andrew Richard Mseya .