Dodoma FM

Serikali kuboresha miundombinu ya mifugo katika ranchi ya Narco

15 March 2023, 6:21 pm

Baadhi ya Ng’ombe wanao patikana katika Ranchi ya Narco iliyopo wilayani Kongwa. Picha na Mariam Kasawa.

Uwekezaji huo wa serikali unalenga kufanya ufugaji wa kisasa zaidi wenye tija ambao utaleta manufaa kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Jumla ya Bilion 4.6 zimewekezwa katika ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Wilayani Kongwa ili kuboresha miundombinu ya Mifungo.

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mifugo Dr Daniel Mushi anazungumzia uboreshaji huo wa miundombinu.

Sauti ya Dr Daniel Mushi

Kwa upande wake Meneja wa Ranchi hiyo ya Taifa Narco iliyopo wilayani Kongwa Bw. Elias Binamungu amesema wananchi wanaozunguka Ranchi hiyo ya Taifa wamenufaika zaidi na vitalu vya ufugaji.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary  Senyamule amesema uwepo wa ranchi hiyo unasaidia kufanya ufugaji wa kisasa na kukabiliana na athari za kutofuga kisasa.

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Ufugaji  ni sehemu ya jadi ya wakazi wengi wa Wilaya ya Kongwa ambayo ni hazina kubwa kwao.