Dodoma FM

DUWASA wapongezwa utekelezaji wa mradi wa visima vya maji Nzuguni

15 March 2023, 11:42 am

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma ikitembelea mradi wa maji wa uchimbaji wa Visima Virefu unaoendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma, (Duwasa).Picha na Seleman Kodima

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma leo imetembelea mradi wa maji wa uchimbaji wa Visima Virefu unaoendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma, (Duwasa) katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma.

Na Seleman Kodima.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma leo imetembelea mradi wa maji wa uchimbaji wa Visima Virefu unaoendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma, (Duwasa) katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma

Pia kamati hiyo imetoa pongeza kwa Serikali na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mkoa wa Dodoma DUWASA kwa hatua kubwa walioifanya katika utekelezaji wa mradi huo

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Jerry Silaa wakati walipotembelea mradi wa visima vitano unaotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA ambapo amesema wameamua kutembelea mradi huo ili kuona zipi changamoto na utekelezaji wake una tija kiasi gani.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Jerry Silaa.

kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA Mhandisi Aron Joseph wakati akisoma muhtasari wa utekelezaji wa mradi huo mbele ya kamati hiyo amesema utambuzi wa eneo hilo ulichangiwa na Viongozi wa mtaa pamoja na Diwani wa kata ya Nzuguni.

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph.

Nae Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma Charles Mamba amewapongeza DUWASA kwa utekelezaji na Usimamizi wa Mradi huo na kuwaomba kuhakikisha wanasimamia ipasavyo muda ulipangwa kumalizika mradi huo ,unafanikiwa.

Diwani wa nzuguni Aloyce Luhega ameiomba Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma kuweza kuukumbuka mradi huo pindi wanapoelekea kwenye bunge la bajeti .

Judith Odunga Rais wa chama cha makandarasi wanawake Tanzania ambaye pia ni Mkandarasi wa Mradi wa huo ameishukuru serikali kwa kuwapa mradi wa nzuguni na kuiomba serikali kuwapatia fedha kwa wakati ili waweze kukamilisha mradi huo kwa muda tarajiwa.

Sauti za Charles Mamba, Aloyce Luhega na Judith Odunga.