Dodoma FM

Wananchi Wahimizwa kufanya utalii wa ndani Jijini Dodoma

14 March 2023, 12:04 pm

Kamishna mwandamizi wa jeshi la uhifadhi Dkt Noelia Mnyonga.Picha na Martha Mgaya

Wananchi Mkoani Dodoma wamehimizwa kuwa na utaratibu wa kufanya utalii wa ndani ukiwemo utalii wa matukio, kwenda maeneo maarufu mkoani hapo, ikiwemo pia na maeneo ya mashamba makubwa yanayolima zao la zabibu.

Na Fred Cheti.

Katika Kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa moja kati ya Mikoa ya kitalii Serikali Mkoani hapa imekuwa ikifanya juhudi na kampeni mbalimbali katika kutangaza vivutio vinavyopatikana Mkoani hapa.

Katika Kuunga Juhudi hizo wageni pamoja na wananchi Mkoani wamehimizwa kuwa na utaratibu wa kufanya utalii wa ndani ukiwemo utalii wa matukio, kwenda maeneo maarufu mkoani hapo ikiwemo pia na maeneo ya mashamba makubwa yanayolima zao la zabibu.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na kamishna Mwandamizi wa jeshi la uhifadhi Dkt Noelia Mnyonga wakati akifanya mahojiano na wanahabari katika ofisi za TANAPA zilizopo Dodoma.

Sauti ya Dkt Noelia Mnyonga.

Moja ya kundi lililosahauliwa katika kufanya utalii wa ndani ni la watu wenye ulemavu ambapo ameelezea mikakati kadhaa katika kusaidia kundi hilo katika kufanya utalii.

Sauti ya Dkt Noelia Mnyonga.