Dodoma FM

Wananchi Bahi waahidiwa kutatuliwa kero zinazowakabili

14 March 2023, 2:34 pm

Akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara Mheshimiwa Gondwe.Picha na Benard Magawa

Kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wa wilaya ya Bahi kutokana na kero zinazowakuta mheshimiwa Godwin Gondwe ameahidi kuyapeleka malalamiko hayo kwenye vikao vya uongozi ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.

Na Benard Magawa.

Kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wa wilaya ya Bahi kutokana na kukosa soko wilayani humo huku wakilalamikia stendi ya Mabasi ya wilaya kujengwa mbali na makazi ya wananchi,

Mkuu wa wilaya hiyo mheshimiwa Godwin Gondwe ameahidi kuyapeleka malalamiko hayo kwenye vikao vya uongozi ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara Mheshimiwa Gondwe amesema atayafanyia kazi maoni na malalamiko yaliyoelezwa na wananchi ili kutatua kero zinazowakabili wananchi huku akiahidi kuanza na suala la soko na stendi ya mabasi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya hiyo mheshimiwa Godwin Gondwe.

Naye Afisa Ardhi wa wilaya ya Bahi Wilbald Ntongani amesema wilaya imetenga eneo la ekari nne karibu na ilipo stendi ya wilaya hivyo hivyo kwa sasa Serikali inasubiri kupata fedha ili eneo la soko liweze kujengwa.

Afisa Ardhi wa wilaya ya Bahi Wilbald Ntongani.Picha na Benard Magawa.

Sauti ya Afisa Ardhi wa wilaya ya Bahi Wilbald Ntongani.

Awali akieleza changamoto ya soko na stendi kwa Mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkazi wa kijiji cha Bahi sokoni wilayani humo Bw. Hamisi Mathias Fungameza ameiomba serikali iruhusu magari madogo kushusha abiria kwenye makazi ya watu badala ya stendi ya mabasi pekee ambayo ipo mbali na makazi huku akiomba soko lijengwe maeneo ya karibu na mikusanyiko ya watu ili biashara zipate wateja.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkazi wa kijiji cha Bahi sokoni wilayani humo Bw. Hamisi Mathias Fungameza.Picha na
Sauti ya Bw. Hamisi Mathias Fungameza.