Dodoma FM

Kamati ya bunge ya utawala yajipanga kuisimamia ofisi ya rais-utumishi

13 March 2023, 3:06 pm

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo. Picha na Utumishi.

kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake ili kuiwezesha kamati yake kutekeleza jukumu la kushauri na kusimamia vema utendaji kazi wa Ofisi ya Rais,

Na Mariam Kasawa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amesema kamati yake imejipanga kikamilifu kutekeleza wajibu wa kuisimamia, kuishauri na kuipa mwongozo sahihi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora .

Mhe. Kyombo amesema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kamati yake na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilicholenga kuwasilisha muundo na majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kwa kamati hiyo.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo

Mhe. Kyombo amesisitiza kuwa, wajumbe wa kamati yake wako tayari kufanya kazi ya kuishauri ipasavyo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake ili kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuujenga Utumishi wa Umma unaowajibika kwa wananchi.

Aidha, Mhe. Kyombo ametoa wito kwa watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake, kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake ili kuiwezesha kamati yake kutekeleza jukumu la kushauri na kusimamia vema utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema watendaji wa ofisi yake wanategemea sana mwongozo wa Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria utakaowawezesha kutekeza majukumu yao kikamilifu ili kufikia lengo la kuboresha utoaji huduma bora kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete