Dodoma FM

Watumishi watakiwa kuimarisha ufanisi katika utendaji

10 March 2023, 3:45 pm

Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu.Picha na Martha Mgaya

Dkt. Jim Yonazi, amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku ili kufanikiwa katika kufikia malengo ya Serikali.

Na Alfred Bulahya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi, amewataka watumishi wa Ofisi hiyo kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku ili kufanikiwa katika kufikia malengo ya Serikali.

Ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum.

Sauti ya Dkt. Jim Yonazi.

Awali, akiongea katika makabidhiano hayo aliyekuwa katibu Mkuu Ofisi hiyo Dkt. John Jingu, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, amewashukuru Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana nae vizuri kwa kipindi chote alichotumikia Serikali katika Ofisi hiyo.

Sauti ya Dkt. John Jingu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa TUGHE katika Ofisi Hiyo Bi. Numpe Mwambenja akitoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa Ofisi hiyo amemshukuru Katibu Mkuu Dkt. Jingu kwa kuwajengea ujasiri na kuondoa uwoga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Sauti ya Bi. Numpe Mwambenja.