Dodoma FM

Nzuguni waeleza kunufaika na Barabara

10 March 2023, 4:37 pm

Baadhi ya wakazi wa Nzuguni Boda wakiwa wanaendelea na shughuli zao mbalimbali. Picha na Thadei Tesha,

Wakazi hao wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara inayoelekea Nzuguni B sambamba na kutoa elimu ya matumizi ya alama za barabarani.

Na Thadei Tesha

Baadhi ya wananchi wanaojishughulisha na biashara mbalimbali katika eneo la Nzuguni Boda jijini Dodoma wamesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara katika eneo hilo imekuwa ni chachu kwa watu kujishughulisha katika fursa za mbalimbali.

Dodoma tv imetembelea katika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wananchi ambapo wanaeleza uwepo wa barabara hiyo umesaidia kwa kiasi gani kuwawezesha wananchi kiuchumi .

Sauti ya wakazi wa Nzuguni Boda.

Pamoja na uwepo wa barabara hiyo baadhi ya wananchi katika eneo hilo wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara inayoelekea Nzuguni B sambamba na kutoa elimu ya matumizi ya alama za barabarani.

Sauti ya wakazi wa Nzuguni Boda.

Eneo la nzuguni jijini dodoma ni kati ya maeneo ambayo yamezungukwa na fursa mbalimbli ambapo wpo baadhi ya wannchi ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.