Dodoma FM

Biashara ya matunda na mbongamboga kuwa mkombozi wa kiuchumi

10 March 2023, 4:10 pm

Biashara ya matunda na mbongamboga.Picha na Martha Mgaya

Biashara ya matunda na mbongamboga katika soko la kizota imetajwa kuwa mkombozi wa kiuchumi kwa baadhi ya wakina mama.

Na Thadei Tesha.

Biashara ya matunda na mbongamboga katika soko la kizota imetajwa kuwa mkombozi wa kiuchumi kwa baadhi ya wakina mama wanaojishughulisha na shughuli za biashara ndogondogo katika soko hilo.

Dodoma FM imefika katika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao na kusema eneo hio limewasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi kwa kuuza bidhaa mbalimbali.

Sauti ya Bi Fatuma.
Sauti ya mama Monica.

Baadhi ya wakina mama hao wameiomba serikali kuwasaidia upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwani mikopo waliyonayo kwa sasa imekuwa ikirudisha nyuma juhudi zao.

Sauti za wakina Mama.

Kizota ni miongoni mwa maeneo ambayo wapo wakina mama ambao wameamua kujiajiri katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara ya kuuza mbogmboga matunda na migahawa.