Dodoma FM

Mkuu wa mkoa wa Dodoma atatua mgogoro wa wakulima na wafugaji

9 March 2023, 12:39 pm

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule akitatua mgogoro wa wakulima na wafugaji.

Mh. Rosemary Senyamule ametatua mgogoro wa wakulima na wafugaji wa vijiji vya Izava na Chitego vilivyopo katika wilaya za Kongwa na Chamwino.

Na Alfred Bulahya.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule ametatua mgogoro wa wakulima na wafugaji wa vijiji vya Izava na Chitego vilivyopo katika wilaya za Kongwa na Chamwino waliokuwa wakigombea eneo la malisho na kilimo.

Mgogoro huo unatajwa kudumu kwa zaidi ya miaka 15 sasa, na umekuwa ukisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo na hata baadhi ya wananchi kuachwa na ulemavu kutokana na mapigano yanayohusisha silaha za jadi.

Akiongea na wakazi wa vijiji hivyo akiwa katika kitongoji cha Wali wilayani Chamwino, Mh Senyamule amewataka wakulima na wafugaji hao kuhakikisha wanatekeleza maelekezo aliyoyatoa na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa kiongozi au mwananchi atakayekwenda kinyume na maelekezo hayo.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, anayekaimu pia wilaya ya Chamwino Remidius Mwema amesema suluhu ya mgogoro huo imetokana na mapendekezo ya vikao mbalimbali vilivyohusisha pande zote mbili.

Sauti ya mkuu wa wilaya Remidius Mwema.

Baadhi ya wakulima na wafugaji kutoka vijiji hivyo wamempongeza mkuu wa mkoa kwa hatua hiyo wakisema wako tayari kutekeleza maelekezo hayo.

Sauti ya wakulima na wafugaji.

Eneo lililokuwa likigombewa lina ukubwa wa zaidi ya hekari 2600.