Dodoma FM

Kituo kidogo cha daladala chatajwa kutoa fursa mbalimbali

9 March 2023, 3:28 pm

Uwepo wa kituo kidogo cha daladala katika eneo la swaswa mnarani jijini dodoma.Picha na Martha Mgaya

Kituo kidogo cha daladala katika eneo la swaswa mnarani jijini dodoma imetajwa kuwa na fursa kubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujipatia kipato.

Na Thadei Tesha.

Uwepo wa kituo kidogo cha daladala katika eneo la swaswa mnarani jijini dodoma imetajwa kuwa na fursa kubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo kujipatia kipato.

Dodoma FM imefika mtaani hapo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wananchi waeneo hilo ambapo wameeleza umuhimu wa uwepo wa eneo hilo kwa kuwakwamua katika shughuli za kiuchumi.

Sauti ya Marco Plilipo.

Wameainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi hao pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na soko la kutosheleza wafanyabiashara ndani ya mtaa huo.

Sauti ya Bw.Abdul

Eneo la swaswa mnarani ni miongoni mwa maeneo maarufu kwa wakazi wa mitaa ya Ilazo mlimwa c na Swaswa ambapo hutumia eneo hilo kwa ajili ya kuvinjari na kufanya manunuzi madogomadogo.

Sauti za wafanyabiashara.