Dodoma FM

Wananchi waingia taharuki kufuatia maeneo wanayomiliki kutaka kuuzwa

8 March 2023, 12:52 pm

Wananchi wa Mitaa wa Chihikwi, Nala, pamoja na Ndachi jijini Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Wananchi wamejikuta wakiingiwa na taharuki kufuatia maeneo wanayoyamiliki yakiwemo mashamba kukutwa yakipimwa na kutaka kuuzwa bila kuwepo kwa taarifa yoyote.

Na Fred Cheti.

Wananchi wa Mitaa wa Chihikwi, Nala, pamoja na Ndachi jijini Dodoma wamejikuta wakiingiwa na taharuki kufuatia maeneo wanayoyamiliki yakiwemo mashamba kukutwa yakipimwa na kutaka kuuzwa bila kuwepo kwa taarifa yoyote.

Sauti za wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri.Picha na Martha mgaya

Kufuata hali hiyo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amefika katika mtaa huo uliopo pembezoni mwa jiji la Dodoma na kuwasikiliza wananchi hao ambao walionekana kuwa na taharuki baada ya kuwaona watu ambao walidai wanatokea halmshauri ya jiji la dodoma kwa ajili ya kupima Maeneo yao bila taarifa.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya ardhi na Mipango miji katika jiji la Dodoma amewataka wananchi hao kufata utaratibu katika kumiliki ardhi ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na umiliki wa ardhi bila utaratibu.

Nae Mwenyekiti wa Mtaa wa Chihikwi anakiri kutokuwa na taarifa zozote juu ya watu hao ambao walionekana wakipima maeneo ya wananchi wake hali iliyozua sintofahamu kwao.

Sauti ya mkuu wa idara na mwenyekiti.