Dodoma FM

Ujenzi wa barabara watajwa kuwa kichocheo cha fursa

7 March 2023, 4:11 pm

Ujenzi wa barabara kuelekea mtaa wa Ntyuka jijini Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Sekta ya barabara imekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa bidhaa.

Na Thadei Tesha.

Ujenzi wa barabara kuelekea mtaa wa Ntyuka jijini dodoma unatajwa kuwa chanzo cha kuchochea zaidi fursa za kiuchumi.

Sauti ya Kashinde Daniell.

hayo ni kwa mjibu wa baadhi ya wananchi wa maeneo hayo walipokuwa wakizungumza na kituo hiki na kusema sekta ya barabara imekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa bidhaa.

Sauti ya James Masai.

kwa upande wao baadhi ya wakina mama pamoja na maafisa usafirishaji katika mtaa huo wamesema kukamilika kwa barabara hiyo kutasaidia kufanya shughuli zao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kupungua kwa gaharama za usafirishaji.

Sauti za wafanyabiashara.

katika mtaa wa Ntyuka maboresho ya barabara yameanza kufanyika kufuatia kuwepo kwa kero ya muda mrefu ndani ya mtaa huo.