Dodoma FM

Tembo wafanya uharibifu wa ekari zaidi ya 100

6 March 2023, 4:46 pm

Moja kati ya shamba lililo haribiwa na Tembo hao wilayani Chemba. Picha na Benard Kapaya.

Tembo hao wamesababisha uharibifu mkubwa katika mashamba hayo na kuwaacha wananchi na sintofahamu.

Na Alfred Bulahya

Kundi la Tembo wanaokadiriwa kuwa zaid ya 300 wamevamia mashamba ya wananchi katika kijiji cha Magungu Kubi katika kata ya Mpendo walayani Chemba na kufanya uharibifu wa mazao ya mahindi zaidi ya hekari 100.

Hayo yamebainishwa leo na Diwani wa kata hiyo Bw Benard Kapaya, wakati akizungumza na Taswira ya Habari kijijini hapo.

Sauti ya Diwani wa kata hiyo Bw Benard Kapaya
Sauti ya Diwani wa kata hiyo Bw Benard Kapaya

Baadhi ya waathirika wa tukio hilo pia wamezungumza na kituo hiki na kueleza uharibifu waliouopata kutokana na uvamizi wa tembo hao katika mashamba yao.