Dodoma FM

WCF kuendelea kuboresha utoaji huduma

3 March 2023, 12:29 pm

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma

Dkt.Mduma amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF huku kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa, huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.

Na Mindi Joseph.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} utaendelea kuboresha utaoji huduma za fidia kwa wafanyakazi nchini wanaopata matatizo ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia walengwa kwa wakati  ili kufikia malengo ya Mfuko huo.

Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo  Machi 2,2023, Jijini Dodoma na kusema hadi kufikia Juni 30 2022 Mfuko umekusanya kiasi cha Shillingi Bilioni 241.48 ikiwa ni kutokana na mapato ya uwekezaji.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma.

Aidha amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa WCF malipo ya fidia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya Shillingi millioni 200 lakini baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huo malipo yanaongezeka kila mwaka.

Sauti ya Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma .