Dodoma FM

Wauzaji wa gesi watakiwa kuwa na mizani ya Vipimo

3 March 2023, 1:14 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri. Picha na Seleman Kodima.

Hayo ameyasema leo wakati akifungua mafunzo ya wafanyabishara wa gesi za kupikia yaliyoandaliwa na wakala wa Vipimo mkoa wa Dodoma ambapo amewataka wakala huo kuhakikisha baada ya siku 60 wafanyabiashara wa gesi za kupikia wanakuwa na mizani ya vipimo sahihi.

Na Selemani Kodima

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri ametoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wa gesi za kupikia jijini Dodoma wawe na mizani ya vipimo ili kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa usahihi wa Vipimo.

Aidha amewataka wananchi kuhakikisha wanapokwenda kununua gesi ya kupikia wawe wanapimiwa katika mizani sahihi ya vipimo na iwapo wanapoona mfanyabiashara hana mizani hiyo watoe taarifa kwa mamlaka ili sheria ichukue mkondo wake.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe Jabir Shekimweri

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Dodoma Karim Zuberi amesema agizo la serikali wamelipokea na kuahidi kuwa wataendelea kutoa elimu kama livyokuwa awali ambapo wamekuwa wakipita kwa wafanyabiashara na kuwakumbusha umuhimu wa mizani .

Sauti ya Meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Dodoma Karim Zuberi

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka wakala mbalimbali wa kampuni za gesi za kupikia wamesema agizo la mkuu wa wilayani ni hatua nzuri ambayo itasaidia kwao na wanunuzi kutambua umuhimu wa kupima mtungi wa gesi kabla kuondoka nao.

Sauti ya washiriki wa mafunzo