

3 March 2023, 2:05 pm
Hatua hii inatoa tafsiri ya moja kwa moja na kuhitaji uhamasishaji wa pamoja wakufikia azma serikali ya Lengo la kupanda miti 5,075,000, katika kipindi cha miaka minne.
Na Selemani Kodima
Wito umetolewa kwa wananchi jijini Dodoma kutumia kumbukizi ya siku zao za kuzaliwa kwa kupanda miti ili kuhakikisha tunafanikiwa kutumiza malengo ya mendeleo Endelevu ya utunzaji wa mazingira
Wito huo umetolewa na Mwalimu Malick Masoud mdau wa mazingira na mratibu wa shirika routs and shoots mkoa wa Dodoma ambaye ameamua kutumia siku yake ya kumbukiza ya kuzaliwa kama sehemu ya kutoa wito kwa jamii kuhusu umuhimu kwa kupanda miti.
Mwl Masoud anasema ameamua kufanya hivyo ili kuonesha umuhimu wa upandaji wa miti kwa jamii na utekelezaji wa vitendo azma ya serikali ya kukijanisha dodoma na sera ya mazingira ya mwaka 2021 ya kuhakikisha kila kaya inapanda miti mitano.
Katika zoezi hilo la upandaji miti ambalo ilikuwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mwl huyo lilihudhuriwa na baadhi ya wadau wa mazingira ,Walimu wa mabingwa wa mazingira kutoka baadhi ya shule jijini Dodoma na hapa baadhi yao wanaelezea lengo la watu kuona umuhimu wa upandaji wamiti.