

3 March 2023, 11:55 am
Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za kimataifa zimejitolea kuleta mabadiliko ya hali hiyo kwa kuanzisha dhana ya wamiliki manufaa.
Na Fred Cheti.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni imesema utoaji wa elimu kwa Wamiliki manufaa umeleta tija katika kuendelea kuhakikisha wanazuia fedha haramu na ufadhili wa kigaidi.
Hayo yamebainshwa jana jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na majina ya biashara Meinrad Rweyemamu katika kikao cha majadiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi.
Amesema Uzoefu unaonyesha kuwa makampuni mengine yamekuwa yakitumika vibaya katika kufanya vitendo vya uhalifu visivyo kubalika kwenye jamii.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Uhamiaji Makao Makuu Dodoma Charles Kasambula amesema elimu hiyo itasaidia katika uchunguzi kwa watu wanaoingia nchini kwa ajili ya shughuli mbalimbali.