Dodoma FM

Nzelenze waiomba serikali huduma ya maji safi na salama

1 March 2023, 5:14 pm

Kisima kidogo kilicho chimbwa katika Korongo kwaajili ya wakazi hao kupata maji. Picha na Mindi Joseph.

Hatua za kukabiliana na changamoto ya maji vijijini bado zinaendelea  ili kuondokana na matumizi ya maji yaliyo tuama na visima vifupi  ambayo ni hatari kwa afya za binadamu.

Na Victor Chigwada                                                              

Wananchi wa kitongoji cha Nzelenze Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuongeza visima vya maji safi na salama  ili kuwasaidia  kuondokana na matumizi ya maji ya visima vya makorongoni.

Wakizunguma na taswira ya habari miongoni mwa wananchi hao wemesema kuwa shida hiyo imekuwa ikiwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata maji ambayo si salama kwao .

Aidha wameomba kusaidiwa na kuongezewa miundombinu ya visima vya maji  yatakayo saidia kutatua changamoto hiyo kwa vitongoji amabvyo havina huduma hiyo ya maji.

Sauti ya Wananchi wa kitongoji cha Nzelenze Kata ya Itiso.
Baadhi ya wananchi wakitoka kuteka maji katika visima vifupi vya korongoni. Picha na Mindi Joseph.

Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni Matambila amekiri changamoto hiyo kuwaathili baadhi ya wananchi wa vitongoji vyake hivyo kupelekea hitaji hilo kuwa kubwa zaidi kwa wananchi

sauti ya Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni Matambila

Matambila ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa visima vya maji safi na salama wanachi wanalazimika kutembea umbali mrefu ili kufuata  maji ya visima vya kuchimba kwa mkono

Sauti ya Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni Matambila