Dodoma FM

Serikali yasaini mkopo nafuu kuboresha huduma za Afya

28 February 2023, 6:18 pm

Naibu Waziri wa Afya Tanzania bara Dkt. Godwin Mollel. Picha na Wizara ya Afya.

Huduma zitakazo boreshwa ni pamoja na kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuboresha huduma za dharura, kuboresha rasilimali watu katika Sekta ya afya, kuboresha utendaji na ufanisi kwenye ngazi ya zahanati.

Na Pius Jayunga.

Serikali ya Tanzania na Banki kuu ya Dunia zimesaini mkopo nafuu utakaosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Hafla hiyo fupi imeongozwa na Waziri wa fedha na mipango nchini Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya bara Dkt. Godwin Mollel aliyemwakilisha Waziri wa Afya pamoja na mwakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Amur Mohamed na viongozi wengine kutoka Wizara ya fedha, Maji na Wizara ya Afya.

Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo amesema nia ya serikali ni kuhakikisha upatikanaji bora wa huduma za afya Nchini hasa katika eneo la afya ya mama na mtoto

Sauti ya Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel.