Dodoma FM

Nollo kumwaga Madawati 800 shule za Msingi

28 February 2023, 4:27 pm

 Mbunge wa Jimbo la Bahi Mkoani Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi Mhe. Kenneth Nollo. Picha na Bernad Magawa.

Halmashauri ya wilaya ya Bahi ambayo kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa na sifa kubwa katika  idara ya elimu Msingi.

Na Bernad Magawaa

MBUNGE wa Jimbo la Bahi . Kenneth Nollo ameahidi kutoa madawati 800 ikiwa ni sehemu ya  kuanza kupunguza changamoto ya upungufu wa Madawati kwa shule za Msingi wilayani humo.

Mheshimiwa Nollo ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika hafla ya  wadau wa elimu iliyofanyika halmashauri  ya Wilaya ya Bahi ambapo ameeleza ukubwa wa tatizo hilo na kuahidi kuanza kulifanyia kazi kupitia fedha za  mfuko wa Jimbo huku akiwaomba wazazi kuungana naye ili kumaliza taizo.

Amesema kuna upungufu wa madawati  9400 kwenye shule za Msingi  katika Wilaya ya Bahi hivyo Ofisi yake imeamua kutoa madawati 800 iwe chachu ya upatikanaji wa madawati yanayohitajika ili kuondoa adha kwa watoto kukaa chini na kurahisisha ujifunzaji wawapo darasani.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Bahi Mh. Kenneth Nollo.
Picha ya Madawati

“ Moja ya changamoto zinazonifanya nishindwe kufanya ziara katika shule za Msingi ni upungufu wa Madawati, naogopa hata kujitambulisha mbele ya watoto mashuleni kuwa mimi ndiye Mbunge wao, nahisi wataniuliza kama wewe ndiye mbunge halafu sisi tunakaa chini unafanya kazi gani?.” Amesema Nollo.

mimi ndiye Mbunge wao, nahisi wataniuliza kama wewe ndiye mbunge halafu sisi tunakaa chini unafanya kazi gani?

Mheshimiwa Nollo amewaomba wananchi na wadau wa elimu waliopo ndani na nje ya Bahi kumuunga mkono kutokomeza kabisa taizo la madawati wilaya ya Bahi ili iwe motisha kwa wanafunzi  na walimu kujituma zaidi na kufanya vizuri kitaaluma.

Amesema pamoja na juhudi za walimu na wanafunzi kuitangaza vema wilaya ya Bahi kwenye suala la elimu katika mkoa wa Dodoma na kitaifa, bado muitikio wa wazazi katika kuchangia masuala  ya elimu siyo mkubwa  hali   inayoweza kuzorotesha juhudi  za watoto na walimu.

“Maeneo mengine wazazi wana muamko mzuri sana katika kuchangia elimu, hata sisi siyo dhambi tukachangia shilingi 5,000/= kwa kila nguvu kazi, naamini tukitoa wote tutatatua changamoto hii, tutaelemishana ili jambo hili liweze kufanikiwa.”  Amesema  Nollo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Bahi Mh. Kenneth Nollo.

Halmashauri ya Bahi ina jumla ya shule 79 zenye jumla ya  wanafunzi  57,209 kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba  ikiwa na madarasa 582 kati ya madarasa 1271 yanayohitajika huku ikikabiliwa na upungufu wa nyumba 1097 za walimu.