Dodoma FM

Wizara ya ardhi yaanza majarabio usalama wa milki za ardhi

24 February 2023, 3:05 pm

Meneja Urasimishaji wa ardhi mijini ambae pia ni Mpimaji mkuu wa ardhi kutoka wizara ya ardhi Bw Leons Peter akizungumza na wananchi. Picha na Seleman Kodima.

Mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi una lengo la kwenda kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki.

Na Selemani Kodima

Wizara ya ardhi kupitia ofisi ya Ardhi mkoa wa Dodoma imeanza majaribio ya mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika mtaa wa Bihawana kata ya Mbabala jijini Dodoma .

Kazi mfano  (Pilot) imeanza  jana huku jiji la Dodoma  likiwa ni sehemu ya Mpango wa ambapo kata  ya kwanza kati ya zile imekuwa ni Mbabala  ndani ya mtaa (Bihawana)

Hayo yamebainishwa  na Meneja Urasimishaji wa ardhi mijini ambae pia ni Mpimaji mkuu wa ardhi kutoka wizara ya ardhi Bw Leons Peter Mwenda wakati akizungumza na wakazi wa mtaa wa Bihawana ambapo ameeleza lengo la Mradi huo na yapi ambayo wananchi wanatakiwa kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.

Sauti ya Meneja Urasimishaji wa ardhi mijini .

Kwa upande wake Afisa mipango miji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bi Anna  Nade  amesema zoezi hilo litawezesha kutambua kila kipande cha ardhi hivyo mwananchi anatakiwa kuonesha ardhi yake na mipaka ya eneo lake.

Sauti ya Afisa mipango miji Bi Anna  Nade.

Naye Afisa Mazingira katoka Halmashauri ya jiji la Dodoma Ally Mfinanga amesema katika hatua ya utambuzi na upimaji wa ardhi hawategemei kupima eneo ambalo ni chanzo cha maji,maeneo ya hifadhi ,milima   huku pia akizungumzia maeneo ya pembezoni mwa barabara yataoteshwa miti .

Sauti ya Afisa Mazingira katoka Halmashauri ya jiji la Dodoma Ally Mfinanga

Mradi wa uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi una lengo la kwenda kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki, kupunguza muda unaotumika kupata nyaraka za milki, kuongeza uelewa wa usalama wa milki kwa kuzingatia jinsia, kuongeza idadi ya watanzania wanaomiliki nyaraka za umiliki pamoja na kuongeza ufanisi utakaofanya wamiliki kuridhika na mchakato wa uandaaji nyaraka za umiliki