Dodoma FM

Wananchi walia na uhaba wa Miundombinu ya Umeme Chiboli

24 February 2023, 4:19 pm

Aina ya Miundombinu ya umeme. Picha na Mtaa kwa mtaa Blog.

Jografia ya kijiji hicho  cha Champumba imekuwa na changamoto katika kusambaza nguzo za umeme licha ya kupewa ahadi ya kusubiri awamu inayofuata.

Na Victor Chigwada.

Kukosekana kwa Miundombinu ya Umeme ikiwemo Nguzo za Kutosha katika Kata ya Chiboli Wilaya ya Chamwino  ni sababu inayosababisha wananchi katika baadhi ya Vitongoji kushindwa kunufaika na nishati hiyo

Hali hiyo imetusukuma kuzungumza na Diwani wa Kata Chiboli  Bw.Wiliamu Teu  ambaye amesema changamoto hiyo ni kilio cha muda mrefu ambapo Mwaka jana walifanikiwa kuunganishia huduma ya umeme

Amesema kuwa licha ya huduma hiyo kuwafikia lakini changamoto iliyoibuka ni kuhusu usambazaji wa nguzo za umeme  kusuasua na  baadhi ya maeneo kwa kutofikiwa na huduma hiyo

Aidha ameiomba Serikali kupitia mamlaka husika kushughulikia changamoto hiyo ili wananchi waweze kunufaika na nishati hiyo ikiwemo kujiletea maendeleo 

Sauti yaDiwani wa Kata Chiboli  Bw.Wiliamu Teu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji amesema kuwa katika kijiji  hicho  kuna vitongoji vitano huku  vitongoji viwili  vikiwa vimefanikiwa kuunganishiwa huduma ya Umeme

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji.