Dodoma FM

Wananchi waelezwa utaratibu wa kupata Hati miliki za Ardhi

23 February 2023, 4:46 pm

Mfano wa Hati miliki ya kimila. Picha na Michuzi Blog

hati miliki zina faida nyingi kwa Serikali na wananchi ikiwemo kupata fursa za mikopo katika ofisi za kifedha.

Na Benadetha Mwakilabi.

Wananchi wameelezwa umuhimu na utaratibu wa kupata hati miliki za ardhi ili ziweze kuwasaidia katika fursa mbalimbali ikiwemo mikopo.

Ni baada ya wananchi wilayani  Kongwa kulalamikia Serikali juu ya suala la upatikanaji wa hati miliki za ardhi Afisa mipango miji wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa Bwana Meshack Silvesta Mlaponi ameelezea utaratibu wa kupata hati hizo.

Akiongea na Taswira ya habari Mlaponi amefafanua mchakato mzima wa muda na gharama za kupata hati miliki hizi

Sauti ya Afisa Mipango Miji Meshack Mlaponi

Aidha Mlaponi amesema hati miliki zina faida nyingi kwa Serikali na wananchi ikiwemo kupata fursa za mikopo katika ofisi za kifedha.

Sauti ya Meshack Mlaponi.

Sambamba na hayo amesema halmashauri ina changamoto ya kushindwa kuvifikia vijiji vyote kwa Mara moja kwaajili ya kutoa elimu na mwitikio mdogo wa wananchi katika kufatilia na kupata hati hizo ambapo ametoa rai yake kwa wananchi kuona umuhimu wa kuandaa hati miliki za ardhi zao.

Sauti ya Meshack Mlaponi .