Dodoma FM

Uongozi umetoa pongezi na shukrani kwa shirika lisilo la kiserikali

21 February 2023, 1:23 pm

Uongozi wa kata ya Chiboli umetoa pongezi na shukrani kwa shirika lisilo la kiserika la Innovation of Africa.Picha na Tanzania homepage

Shirika lisilo la kiserika la Innovation of Africa limepongezwa na Uongozi wa kata ya Chiboli kwa juhudi zake wanazozifanya za kutatua changamoto.

Na Victor Chigwada.

Uongozi wa kata ya Chiboli umetoa pongezi na shukrani kwa shirika lisilo la kiserika la Innovation of Africa kwa juhudi zake wanazozifanya za kutatua changamoto ya upatikanji wa huduma ya maji maeneo ya Vijijini

Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya Viongozi wa Vijijini vinavyopatikana katika kata ya Chiboli ambapo Taswira ya Habari imezungumza na Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji ambapo amesema.

“licha ya changamoto ya uwepo wa changamoto ya maji kijijini hapo lakini shirika la Innovation of Africa wamefanikiwa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama ili kuondokana na matumizi ya maji ya bwawani”

Shirika la Innovation of Africa wamefanikiwa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama ili kuondokana na matumizi ya maji ya bwawani”

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji.

Mdabaji ametoa shukrani zake kwa shirika hilo kwani wamekuwa msaada kwa wananchi tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanategemea maji ya bwawani ambayo yaliwasababisha magonjwa mbalimbali.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Champumba Bw.John Mdabaji.

Nae Diwani wa Kata ya Chiboli Bw. Wiliamu Teu amesema licha ya hatua hizo ,lakini bado kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya maji hivyo wanaendeela kuhakikisha wanaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Aidha diwani huyo amewaomba Serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia kuongeza idadi ya visima ndani ya vitongoji vya kata ya chiboli ili kuepukana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji safi na salama.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Chiboli Bw.Wiliamu Teu.

“Licha ya hatua hizo bado kata ya chiboli inakabiliwa na changamoto ya maji hivyo wanaendelea kuhakikisha wanaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama”