Dodoma FM

Kuibuka kwa wimbi kubwa la matapeli kwa njia ya mitandao ya simu

21 February 2023, 2:25 pm

Vitendo vya utapeli wa mtandaoni ambapo wamesema kuwa aina hii ya utapeli kupitia simu za mkononi imewasababisha athari.Picha na Mwananchi

Kuibuka kwa wimbi kubwa la matapeli kwa njia ya mitandao ya simu ,imetajwa kusababisha baadhi ya watu kupoteza fedha na mali kwa watu wasiojulikana.

Na Victor Chigwada.

Hayo yamefahamika baada ya Taswira ya Habari kuzungumza na Baadhi ya wananchi wa Kata ya Itiso Wilaya ya Chamwino kujua namna gani wamekuwa wakiripoti vitendo vya utapeli wa mtandaoni ambapo wamesema kuwa aina hii ya utapeli kupitia simu za mkononi imewasababisha athari baadhi ya watu hivyo Serikali waendelea kuwadhibiti vitendo hivyo.

“Pia wamesema iwapo Jeshi la Polisi litasimamia imara na kuwakamata wahusika vitendo hivyo itasaidia kukomesha wimbi kubwa la wizi huo ambao umeshika kasi kwa hivi sasa.”

Mwananchi.

Pamoja na hayo wamesema ushirikiano baina ya jeshi la Polisi ,Mamlaka ya mawasiliano Taania TCRA na Makampuni ya mawasiliano ya Simu kwa Pamoja yanaweza kudhibiti vitendo vya utapeli wa njia ya mtandao.

Mwananchi

Naye Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni Matambila ametoa ushuhuda wa utapeli ulitokea ndani ya kata hiyo na kusababisha hasara ya kupoteza kiasi kikubwa cha fedha.

Diwani wa Kata ya Itiso Bw.Simoni.

Mwaka jana Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilizindua kampeni ya elimu kwa umma ikiwa na lengo la kuwakumbusha na kuwaelimisha watumiaji wa huduma za mawasiliano na wananchi umuhimu wa kutumia huduma hiyo kwa umakini ili kuepuka wizi na ulaghai wa kimtandao.