Dodoma FM

Mashekhe watakiwa kufanya kazi kwa weledi

20 February 2023, 4:20 pm

BAKWATA ngazi ya Mkoa wa Dodoma .Picha na fullblog habari.

Baadhi ya mashekhe wa kata wameshindwa kuwa na fikra ya utatuzi wa baadhi ya changamoto katika jamii ikiwemo masuala ndoa, migogoro ya kifamilia na kuwa na njia ya kuhakikisha ofisi za kata zinapatikana

Na Seleman Kodima.

Baraza la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Dodoma Mjini limeendelea kupigilia msumaria kauli ya Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally kuwa haitoweza kuwavumilia mashekhe watakaoshindwa kuhudumia jamii na serikali .

Kauli ya Mufti Mkuu wa  Tanzania inawapa nafasi  Bakwata kutoweza  kuvumilia na kufanya kazi na mashekhe wasioweza kwenda na kasi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Bakwata  wilaya ya Dodoma  Bashiru Ally Hussein wakati akizungumza hatua ya utekelezaji juu ya  kauli ya Mufti Mkuu wa  Tanzania ambayo inasema badilikia, jitambue acha mazoea, amesema kauli hiyo inawapa nafasi  Bakwata kutoweza  kuvumilia na kufanya kazi na mashekhe wasioweza kwenda na kasi ya kuhuduma jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri Bakwata  wilaya ya Dodoma – Bashiru Ally Hussein