Dodoma FM

Wakurugenzi watakiwa kutumia data za sensa kupanga sera na mipango

17 February 2023, 11:49 am

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa. Picha na African press

Wakurugenzi wa sera na mipango wametakiwa kuhakikisha wanatumia data za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kupanga mipango jumuishi.

Ofisi ya taifa ya Takwimu imewataka wakurugenzi wa sera na mipango kuhakikisha wanatumia data za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kupanga mipango jumuishi ili wananchi waanze kunufaika na Takwimu hizo.

Hayo yamesemwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa wakati akizungumza na wakurugenzi hao waliokutana jijini Dodoma kujadili viashiria vya mipango ya maendeleo ya taifa kikanda na kimataifa zinazoweza kujibiwa na takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Dkt. Chuwa